ATHENS-UGIRIKI

Viongozi wa serikali ya Ugiriki wakutana kujadili swala la kuomba mkopo kutoka IMF

viongozi wa serikali ya Ugiriki
viongozi wa serikali ya Ugiriki

Viongozi wa Serikali ya Umoja ya Ugiriki wanakutana kwa mara ya tatu hii leo kwa ajili ya kujadili utekelezaji wao katika kuhakikisha wanapata mkopo wa euro bilioni kumi na moja nukta tano kutoka Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha Duniani IMF. 

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hawa wanakutana ili kuhakikisha mkakati wao wa kupata mkopo kutoka EU na IMF unafanikiwa ili kujiepusha na hali mbaya ya kiuchumi ambayo wanakabiliwa nayo kwa sasa.

Naibu waziri wa Fedha Christos Staikouras amesema wameshapiga hatua nzuri na anamini Viongozi hao watakubaliana katika utekelezaji wa kile ambacho wamekipanga ili kufanikisha malengo yao.

Miongoni mwa vitu ambavyo Viongozi hao wanastahili kukubaliana ni pamoja na kubana matumizi ili kutekeleza moja ya sharti la Umoja wa Ulaya EU ili waweze kupata mkopo huo na kupiga hatua.

Mkutano huu unakuja siku kadhaa baada ya Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya EU kutembelea Athens na kuitaka serikali kuhakikisha inaonesha njia ya kukabiliana na hali ngumu na kudorora kwa uchumi.