YEMEN

Shambulizi la kujitoa mhanga laua watu 20 nchini Yemen

Wanamgambo wa Al Qaeda wanaodaiwa kufanya shambulizi la kujitoa mhanga nchini Yemen
Wanamgambo wa Al Qaeda wanaodaiwa kufanya shambulizi la kujitoa mhanga nchini Yemen latimesblogs.latimes.com

watu 20 wameuawa kusini mwa Yemen na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa baada ya shambulizi la kujitoa mhanga kutekelezwa na wapiganaji wanaosadikiwa kuwa ni Alqaeda.

Matangazo ya kibiashara

Gavana wa jimbo la kusini mwa Yemen Jamal al-Aqal amethibitisha taarifa hizo zilizotumwa kupitia mtandao wa wizara ya ulinzi.

Aidha katika tukio jingine mashariki mwa Yemen kunasadikika majeshi ya Marekani yamewashambulia na kuwaua wanamgambo 5 wa Alqaeda siku ya jumamosi.

Mamlaka husika imeanza upelelezi ili kubaini idadi kamili ya vifo sambamba na wahusika wa tukio la shambulizi hilo.