Egypt

Marekani na Misri zafanya majadiliano kuhusu msaada wa usalama huko Sinai

abcnews.go.com

Marekani na Misri zinafanya majadiliano kujaribu kuweka pamoja mpango mpya wa msaada wa usalama katika kusaidia kushughulikia hali mbaya ya machafuko iliyojitokeza huko Sinai. 

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gazeti la New York Times ,Jeshi la Misri limekuwa likiimarisha uwepo wake katika eneo la Sinai kwa mizinga na helikopta baada ya tukio la uvamizi mpakani jirani na mpaka wa Gaza na Israel Jumapili iliyopita , tukio lililosababisha vifo vya askari 16 wa Misri.

Wanamgambo wa Kiislamu, ambao walifanya mashambulizi, wanaaminika kuwa na uhusiano na Jeshi la kiiislamu, kundi dogo la waislam wenye msimamo mkali ambalo limekuwa likishutumiwa na Misri kwa mashambulizi kadhaa katika miaka ya nyuma.