IRAN-TETEMEKO LA ARDHI

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na matetemeko pacha ya ardhi nchini Iran yaongezeka

Baadhi ya waathirika wa tetemeko la Ardhi nchini Iran
Baadhi ya waathirika wa tetemeko la Ardhi nchini Iran nydailynews.com

Shughuli za uokozi wa watu waliofunikwa na vifusi baada ya kutokea matetemeko pacha ya ardhi ambayo yamepiga katika Mkoa wa Tabriz kaskazini magharibi mwa Iran, siku ya Jumamosi. Awali iliripotiwa kuwa takriban waru 220 ndio amvbao walipoteza maisha huku watu 1.500 wakijeruhiwa. idadi hiyo imeongezeka kufikiaa watu 227, huku watu zaidi ya 200 wakijeruhiwa.   

Matangazo ya kibiashara

Waokozi wametangza kusitisha huduma za ukozi, huku wakifahamisha kwamba wamejairbu kuokowa watu waliokuwa wamefunikwa katika vifusi katika vijiji vya Ahar na Varzaghan.

Hossein Ghadami mfanyakazi kwenye wizara ya mambo ya ndani anaehusika na maswala ya majanga amesema kwamba serikali inajaribu kuhakikisha huduma inawafikia waathiriwa wa janga hili, ambapo juhudi zaidi zinahitajika katika kuwahifadhi watu wanaoendelea kulala barabara kwa hofu ya kutokea tena kimbunga.

Kijiji cha Varzaghan kilicho kwenye umbali wa kilometa 60 na mji wa Tabriz, ndicho kinacho tanjwa kuathirika zaidi kutokana na matetemeko hayo pacha ya  hilo la ardhi.

Hospitali mbalimbali katika maeneo hayo zimefurika majeruhi ambao wengi wanaendelea kupanga foleni wakisubiri kupewa huduma.

Matetemeko hayo pacha yaliyopiga kwa dakika 11 kila moja yalikuwa na ukubwa wa kipimo cha 6.2 na 6.0 kwa mujibu wa chuo kikuu cha Tehran.