YEMEN

Watuhumiwa sita wa Alqaeda washikiliwa na polisi Yemen

AFP

Jeshi la usalama nchini Yemen linawashikilia watuhumiwa sita wa kundi la alqaeda akiwemo imamu wa msikiti katika mji wa kusini wa Aden baada ya kuwepo mashambulizi yaliyopoteza maisha ya askari kumi na tisa hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Wana usalama hao walifanikiwa kuivamia nyumba moja mjini Aden na kuwakamata watuhumiwa watatu na imam wa msikiti akitiwa nguvuni baada ya kukutwa nyumbani kwake.

Wakielezea kwa masharti ya kutotaja majina wanausalama hao wamesema watuhumiwa wengine wawili walikamatwa mapema alhamisi na zoezi la kuapambana na kundi hilo litakuwa endelevu kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni katika makao makuu ya usalama nchini huyo yaliyoua askari kumi na tisa.

Kufuatia hali hiyo jeshi la usalama nchini humo limeongeza vituo vipya sita katika jiji hilo ili kuhakikisha usalama unakuwepo.