UGANDA

Jeshi la Uganda lakabiliana na waasi wa LRA laua wawili

Waasi wa LRA wanaopambana dhidi ya  majeshi ya serikali ya Uganda
Waasi wa LRA wanaopambana dhidi ya majeshi ya serikali ya Uganda AFP PHOTO/STRINGER

Wanajeshi wa Uganda wanaomtafuta kiongozi wa kundi la waasi la LRA Joseph Kony wamekabiliana na wafuasi wa kundi hilo na kuwaua waasi wawili.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la Uganda,Felix Kulayigye amesema makabiliano hayo yalizuka Ijumaa iliyopita msituni katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kulaiyge ameongeza kuwa jeshi la Uganda limemwokoa mtoto wa miaka sita kutoka Uganda pamoja na mtu mtu mwingine mwenyewe umri wa miaka 19 kutoka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Joseph Kony kiongozi wa kundi hilo anatakiwa na Mahakama ya kimataifa ya ICC mjini Hgaue kwa makosa ya mauji na visa vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Mpaka sasa inaaminika kuwa takribani wapiganaji 250 wamechukuliwa kujiunga jeshi hilo dhidi ya majeshi ya serikali ya Uganda huku kundi hilo likiendelea kuvuma kwa kutorosha watoto na kuwatumia kama wabeba mizigo na watumwa wa ngono.