CAMEROON-NIGERIA

Mafuriko yaua Nigeria baada ya Mvua kupiga nchi jirani ya Cameroon

Mafuriko nchini Nigeria yaharibu takribani vijiji 40 huku idadi ya watu kadhaa bado hawaonekani
Mafuriko nchini Nigeria yaharibu takribani vijiji 40 huku idadi ya watu kadhaa bado hawaonekani viewtz.com

Takriban watu kumi wamepoteza maisha mashariki mwa Nigeria huku wengine elfu 20 wakiachwa bila makazi baada ya kutokea mafuriko nchini humo baada ya mvua kubwa kunyesha nchi jirani ya Cameroon.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa shirika la kudhibiti majanga katika jimbo la Adamawa nchini Nigeria Shadrach Daniel, amesema kuwa maji hayo yalitokea katika bwawa na kuharibu vijiji zaidi ya 40 na kuongeza kuwa mpaka sasa watu wengine hawajulikani walipo.

Takriban watu ekfu 20 wamepatiwa hifadhi katika kambi za muda mfupi ambapo watu hao wamekuwa wakihitaji maji, chakula, mavazi na mablanketi.

Maji hayo yalitoka katika bwawa la Lagdo nchini Cameroon siku ya ijumaa baada ya maafisa nchini humo kuionya Nigeria majuma kadhaa yaliyopita, kufunguliwa kwa Bwawa hilo kulisababisha mafuriko katika eneo la mto Benue nchini Nigeria.