Afrika Kusini

Matumaini yaonekana mzozo wa wafanyakazi na wamiliki wa kampuni ya madini ya fedha nchini Afrika Kusini.

Jo Soeka, mpatanisi wa mzozo wa Afrika Kusini
Jo Soeka, mpatanisi wa mzozo wa Afrika Kusini geoconger.wordpress.com

Kampuni ya tatu duniani kwa uzalishaji wa madini ya fedha nchini Afrika Kusini Lonmin , pamoja na wapatanishi wa mgogoro baina ya kampuni hiyo na wafanyakazi wake, wamekuwa na matumaini ya kufanikiwa katika mazungumzo na wafanyakazi hii leo na kumaliza mgomo wa wiki tatu baada ya ghasia ziliosababisha watu 44 kupoteza maisha. 

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yaliyoandaliwa na viongozi wa serikali ya Afrika Kusini yalianza baada ya pande mbili kukutana kwa saa 12 siku moja kabla, katika mji wa kaskazini Magharibi wa Rustenburg.

Akizungumza na shirika la habari la Ufaransa AFP mpatanishi wa mzozo huo Askofu Jo Seoka kutoka baraza la makanisa la Afrika Kusini amesema kuwa anadhani leo itakuwa siku ya kuamua jinsi ya kusonga mbele huku msemaji wa kampuni hiyo Sue Vey akisema kuwa upatanishi wa serikali ni wa kujenga.

Kampuni hiyo inataka mkataba wa amani utakao unganisha pande zote kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu madai ya mshahara ya wafanyakazi lakini wafanyakazi wanasisitiza hawawezi kurudi kazini hadi madai yao yatakapotimizwa..