SYRIA

Wanajeshi zaidi ya 8000 wameuwawa nchini Syria tangu kuanza kwa machafuko.

Mmmoja wa askari majeruhi akiwa katika hospitali ya Tishrin mjini Damascus.
Mmmoja wa askari majeruhi akiwa katika hospitali ya Tishrin mjini Damascus. washingtonpost.com

Zaidi ya wanajeshi 8,000 wa vikosi vya usalama wameuwawa nchini Syria tangu kuanza kwa mapambano dhidi ya utawala wa Syria na waasi mwezi Machi mwaka 2011, mkurugenzi wa hospitali ya jeshi ya Tishrin amesema. 

Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi huyo ambaye pia ni daktari amesema kuwa kila siku wamekuwa wakipokea wastani wa miili 15 hadi 20 ya askari na wanachama wa vikosi vya usalama, huku idadi hiyo ikiongezeka tangu mwanzo wa mwaka.

Hospitali ya Tishrin imepokea miili 47 siku ya Jumatano, lakini mwishoni mwa mwezi Julai wakati mapigano katika mji mkuu yakiendelea wakati waasi wakijaribu kudhibiti eneo hilo, hospitali hiyo ilipokea zaidi ya watu 100 kila siku kwa siku tatu, amesema daktari huyo.

Kulingana na ripoti ya waangalizi wa haki za binadamu nchini humo, askari karibu 6,500 na wanachama wa vikosi vya usalama wameuawa katika kipindi cha miezi 17, nje ya jumla idadi ya vifo vya watu zaidi ya 25,000, wengi wao wakiwa raia.