Pata taarifa kuu
IRAN

Malumbano kuhusu nuklia yatawala mkutano wa Iran.

saidaonline.com
Ujumbe kutoka: Sabina Chrispine Nabigambo
1 Dakika

Mkutano wa Nchi zisizofungamana na upande wowote unaofanyika mjini Tehran nchini Iran ulionekana kuanza na malumbano mara tu ulipoanza baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuishinikiza Tehran kuhusu msimamo wa nchi hiyo katika mpango wake wa Nuklia. 

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa kidini nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei alifungua mkutano huo kwa hotuba iliyokuwa ikiikemea Marekani kuwa imekuwa ikiingilia masuala ya Iran na kuukosoa utawala wa Israel.

Khamenei ameitetea nchi yake kuwa haina mpango wa kutengeneza silaha za Nuklia na kulishutumu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kutoitendea haki Iran kwa shinikizo la Marekani na njama zake alizoziita za udiktekta duniani.

Ban Ki Moon aliyeonekana kukerwa na hotuba ya Khamenei ameitaka Iran kuonesha dhamira yao ya usalama katika mpango wake wa Nuklia na kurudisha imani hiyo kimataifa kwa kufuata maazimio ya Baraza la usalama na kutoa ushirikiano na shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki IAEA.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.