Rwanda-DRCongo

Rwanda yakaza uzi kutohusika na machafuko DRC

Rais wa Rwanda Paul Kagame .
Rais wa Rwanda Paul Kagame . AFP PHOTO / STEPHANIE AGLIETTI

Nchi ya Rwanda inaendelea kujitetea kutohusika na mgogoro unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha ya ripoti ya Umoja wa mataifa, na kuendelea kuchukulia madai hayo ya ripoti kuwa ni tuhuma zisizo na msingi wowote wa kuthibitika. 

Matangazo ya kibiashara

Nchi ya Congo inatoa msisitizo kuwekwa vikwazo dhidi ya Rwanda pamoja na harakati zinazoendelea kwa upande wa Viongozi wa dini na mashirika ya kiraia kuomba nchi ya rwanda ishiriki kikamilifu kutafuta suluhu ya mgogoro baina ya serikali ya DRC na waasi wa M23.

Wachambuzi wa maswala ya siasa wanaona kuwa hali hii ya serikali ya Rwanda ni kiini macho tu, na kusema kuwa sababu za kuhusika kwa nchi hiyo katika Mgogoro wa Congo ni za kiuchumi.

Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa ikiishutumu nchi ya Rwanda kufadhili makundi ya waasi Mashariki mwa nchi hiyo.