SYRIA

Syria yaishukia Uturuki kuhusu ugaidi

breakingnews.sy

Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Syria ameishutumu vikali Uturuki kwa kuwapa mafunzo na kuwezesha upenyaji wa magaidi , kulingana na mahojiano ya televisheni yaliyotolewa wakati wa mkutano wa kilele wa mataifa yasiyo fungamana na upande wowote huko Iran. 

Matangazo ya kibiashara

Naibu waziri Faisal Muqdad ameiambia televisheni ya kiarabu ya Al- Alam kuwa Uturuki ina jukumu la uharibifu katika mzozo huo na kwamba kwamba imekuwa ikwtoa mafunzo na kuruhusu magaidi hasa wa kundi la Al Qaeda.

Faisal ameongeza kuwa suala hilo inabidi kujadiliwa kwa sababu endapo Uturuki haitaitikia suala hilo , hivyo itabidi nchi hiyo iwekwe katika orodha ya mataifa yanayounga mkono ugaidi.

Muqdad amesema sera za Ankara kuhusu Syria zinaendeshwa kinyume na maslahi yake yenyewe, na hivyo kuitaka serikali ya Uturuki kurejea katika fikra zake.