Marekani

Marekani yasema haitoendelea kuvumilia wanaotumia mwanya wa maandamano ya kidini kutekeleza mashambulizi dhidi ya balozi zake

Serikali ya Marekani imetangaza kutoendelea kuwa na uvumilivu na wale wote wanaotumia mwanya wa kidini kutekeleza mashambulizi dhidi ya Balozi zake hasa mashariki ya kati na Kaskazini mwa Afrika. Waandamanaji wenye hasira waliharibu gari za ubalozi wa Marekani jijini Sanaa nchini Yemen, huku jijini Kairo hali ikiendelea kupamba moto.

waandamanaji wakiandamana katika jiji la Sanaa, nchini Yemen polisi ililazimika kutumia nguvu bila mafaaniki wakati waandamanji walipo vamia ubalozi wa marekani
waandamanaji wakiandamana katika jiji la Sanaa, nchini Yemen polisi ililazimika kutumia nguvu bila mafaaniki wakati waandamanji walipo vamia ubalozi wa marekani REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Marekani imesema itafanya kila linalowezekana kulinda raia wake katika nchi hizo na wametoa wito kwa Viongozi wa Serikali na Jamii na Dini hususani nchini Misri kukomesha machafuko kama anavyoeleza Waziri wa Mambo ya Nje Hillary Clinton.

Katika hatua nyingine serikali ya Libya imetangaza kuwashikilia watuhumiwa waliohusika kwenye mauaji ya Balozi wa Marekani na tayari Waziri Mkuu Mustafa Abu Shagour amesema wataendelea kushirikiana na serikali ya Washington.

Maandamano ya kupinga filamu inayoelezwa kumdhihaki Mtume Muhammad (s.a.w) yameendelea katika nchi zenye waislam wengi na kwenda kufanya mashambulizi kwenye Balozi za nchi hiyo.

Baada ya Libya, Misri, Yemen, wananchi katika nchi mbalimbali za kiislam wameandaa maandamano leo baada ya sala ya Ijumaa. Balozi za nchi za magharibi katika nchi za Afghanistani, Pakistani zimechukuwa hatuwa za tahadhari dhidi ya maandamano hayo na kuwataka watu wake kutotembea leo siku ya Ijumaa.