CHINA-JAPAN

Mgogoro wa kuwania Kisiwa baina ya Japan na China watishia uhusiano wa kidplomasia baina ya mataifa hayo

Waandamanaji nchini China ambao wanadai umiliki wa Kisiwa cha Senkaku kinachomilikiwa na Japan
Waandamanaji nchini China ambao wanadai umiliki wa Kisiwa cha Senkaku kinachomilikiwa na Japan REUTERS/Jason Lee

Uhusiano baina ya China na Japan unaelekea kuzidi kuharibika kutokana na kushuhudiwa kwa kauli zinazodhihirisha hali si shwari baina ya nchi hizo kipindi hiki ambacho huko Beijing kuna maandamano yanayoenda sambamba na kushambuliwa kwa viwanda ambavyo vinamilikiwa na Tokyo.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji wameendelea kushambulia mali ambazo zinamilikiwa na serikali ya Japan na wafanyabiashara kutoka nchi hiyo kutokana na uwepo wa mgogoro baina ya nchi hiyo na China juu ya umiliki wa Kisiwa ambacho Taiwani nao wanadai ni mali yao.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Hong Lei amesema wao wataendelea kulinda mali zinazomilikiwa na Japan lakini amekataa kushushiwa tuhuma za wao kuwa chanzo cha maandamano na kuharibiwa kwa mali hizo.

Viwanda kadhaa vinavyomilikiwa na Japan vimesimamisha kazi zake kutokana na mashambulizi hayo ambapo Kampuni ya vifaa vya kamera Canon, Kampuni ya vifaa vya umeme Canon na kampuni ya magari ya Toyota Motor ni miongoni mwa waliosimamisha shughuli zao.

Wakati hali inaonekana inazidi kuwa mbaya kwenye uhusiano wa China na Japan ndipo Waziri wa Ulinzi wa Beijing Jenerali Liang Guanglie amesema wao wataendelea na hatua zaidi za kuhakikisha wanapata suluhu ya mgogoro huo wa mipaka.

Jenerali Guanglie amesema serikali yake inafuatilia hali inavyoendelea kwenye Kisiwa hicho kilichopo Mashariki mwa China na wanahaki ya kufanya lolote ili kurejesha kwenye himaya yao eneo hilo.

Waziri huyo wa Ulinzi licha ya kutamba kuwa wanaweza kutumia nguvu na wana haki ya kufanya hivyo lakini ameendelea kusisitiza wanataka njia ya mazungumzo itumike kumaliza mgogoro huo wa mipaka.

Kisiwa hicho kina majina mawili kwani Japan wenyewe wanakitambua kwa jina la Diaoyu huku wenzao China wao wanakiita Senkaku na kwa sasa kipi chini ya japan licha ya kuwania na Taiwan pia.