Pata taarifa kuu
CHINA-JAPAN

China yapeleka meli nyingine mbili jirani na visiwa Senkaku vyenye mgogoro kati yake na nchi ya Japan

Visiwa vya Senkaku ambavyo vinagombewa na nchi za China na Japan
Visiwa vya Senkaku ambavyo vinagombewa na nchi za China na Japan Reuters
Ujumbe kutoka: Emmanuel Richard Makundi
1 Dakika

Serikali ya China imetuma meli nyingine mbili za uchunguzi kwenye eneo la kisiwa chenye mgogoro kati yake na nchi ya Japan katika kile kinachoelezwa ni kuangalia iwapo Japan inafanya shughuli zozote kwenye kisiwa hicho wakati bado hakuna muafaka.

Matangazo ya kibiashara

Shirika la habari la Uchina, Xinhua limethibitisha kupelekwa kwa meli hizo jirani na kisiwa cha Diaoyu ikiwa ni moja ya hatua za kuhakikisha nchi ya Japan licha ya kununua visiwa hivyo haifanyi shughuli zozote.

Kwa mujibu wa Serikali ya Japan, imethibitisha kushuhudia meli hizo mbili na kuongeza kuwa zimevuka eneo lake la bahari na kuingia hadi nchi ya Japan hali inayohatarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Nchi hizo mbili kila mmoja imekuwa ikidai ni mmiliki wa halali wa visiwa hivyo, visiwa ambavyo hata nchi ya Taiwani nayo imedai kuwa ni mmiliki halali wa visiwa vinavyogombewa na nchi hizo.

Majuma kadhaa yaliyopita yameshuhudiwa maandamano makubwa nchini China dhidi ya Serikali ya Japan wakidai kuwa nchi hiyo inataka kutumia mabavu kujimilikisha visiwa hicyo kinyume cha sheria.

Maandamano hayo yalisababisha makampuni kadhaa ya Japan kufunga ofisi zake nchini China baada ya waandamanaji kuvamia ofisi hizo na kuharibu baadhi ya Mali.

Jumuiya ya kimataifa imetaka nchi hizo kurejea kwenye meza ya mazungumzo kumaliza tofauti zao kuhusu visiwa hivyo ambavyo vinaelezwa kuwa na utajiri wa Gesi na Mafuta.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.