UHISPANIA

Hali ya usalama yaanza kurejea mjini Madrid, Hispania baada ya maandamano ya wananchi

Maelfu ya waandamanaji nchini Hispani wakiwa kwenye uwanja wa Madrid
Maelfu ya waandamanaji nchini Hispani wakiwa kwenye uwanja wa Madrid Reuters

Polisi nchini Uhispania wametumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kiwatawanya maelfu ya waandamanaji nchini humo waliojitokeza barabarani kupinga mpango wa serikali wa ubanaji matumizi.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanji hao walilizunguka bunge la nchi hiyo mjini Madrid wakiushutumu utawala wa nchi hiyo kwa kushindwa kushughulikia vizuri tatizo la mdororo wa kiuchumi ambao umeendelea kuikabili nchi hiyo.

Wananchi hao pia wametaka kuitishwa kwa uchaguzi mkuu mpya nchini humo utakaopelekea kuundwa kwa Serikali mpya wakidai Serikali iliyoko sasa imeshindwa kazi ya kumaliza matatizo ya uchumi nchini humo.

Waandamanji hao pia wanapinga mpango wa Serikali wa kuondoa pensheni kwa wafanyakazi wa Serikali, jambo ambalo waziri mkuu Mariano Rajoy amekanusha kuwa Serikali yake itatekeleza mpango huo.

 

Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa kwenye maandamano hayo wakiwemo Polisi huku waandamanaji hao wakidai kuendelea na maandamano yao kwa siku ya pili mfululizo.