Pata taarifa kuu
VENEZUELA

Rais Hugo Chavez avitaka vyama vya siasa kukubali matokeo ya uchaguzi unaofanyika leo.

Rais wa Venezuela  Hugo Chavez
Rais wa Venezuela Hugo Chavez RFI/Keo Chhaya
Ujumbe kutoka: Sabina Chrispine Nabigambo
1 Dakika

Rais wa Venezuela Hugo Chavez ametoa wito kwa vyama vyote vya siasa nchini humo, kukubali matokeo ya uchaguzi wa rais unaofanyika leo Jumapili, akisema matokeo hayo hayata maanisha mwisho wa dunia kwa mtu yeyote. 

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mazungumzo na mkuu wa ujumbe wa wataalamu wa uchaguzi toka Marekani Kusini,Carlos Alvarez, rais Chavez amezitaka pande zote kukubali matokeo yatakayo tangazwa na Baraza la Taifa la Uchaguzi.

Kiongozi huyo maarufu wa mrengo wa kushoto anakabiliwa na upinzani mkali akiwa madarakani kwa karibu miaka 14 ,toka kwa mgombea wa upinzani Henrique Capriles, ambaye alikuja juu katika kura za maoni lakini akaachwa nyuma kwa alama kumi katika utafiti wa karibuni.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.