Venezuela

Hugo Chavez ashinda uchaguzi Venezuela, upinzani wakubali matokeo

REUTERS/Jorge Silva

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Venezuela imemtangaza Hugo Chavez kama mshindi wa kinyang'anyiro cha uchaguzi wa urais uliofanyika siku ya jumapili na hivyo kupata kipindi kikingine cha miaka sita kuongoza taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

 Uchaguzi huo ambao ulivuta hisia za watu wengi umeshuhudia maelfu ya wananchi wakijitokeza kupiga kura tofauti na miaka mingine ambapo watu hawakujitokeza kama safari hii.

Tayari aliyekuwa mgombea wa upinzani kwenye uchaguzi huo na kuungwa mkono na vyama zaidi ya 30 vya upinzani Henrique capriles amempongeza rais Chavez kwa ushindi huo.

Akiwahutubia wafausi wake mjini Caracas, Capriles amesema amejifunza mengi kutokana na uchaguzi huo na kwamba ana imani siku moja upinzani utachukua dola.

Chavez ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 54.42 wakati mpinzani wake Capriles amepata asilimia 44.97.