LIBYA-MAREKANI

Marekani yatoa ripoti mpya kuhusu kulipuliwa kwa ubalozi wake nchini Libya

AFP PHOTO/GIANLUIGI GUERCIA

Maafisa wa Marekani wametoa ripoti yao kuhusu tukio la uvamizi na kuchomwa moto kwa ubalozi sake mjini Bengazi nchini Libya na kusababisha madhara makubwa pamoja na vifo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti inaonyesha kuwa watu kadhaa wenye silaha walivamia Ofisi ndogo ya ubalozi mjini Banghazi mwezi uliopita na kuchoma moto ofisi hiyo.

Uvamizi huo ulisababisha vifo vya wamarekani wanne akiwemo Balozi wa Marekani nchini Libya, maafisa wa Marekani wameeleza.

Ripoti ya maafisa hao wa marekani imeeleza kuwa hakuna onyo lolote lililotolewa na ofisi ya kiintelijensia kuwa kulikuwa na shambulio hata baada ya shambulio hilo
Maafisa hao wamesema kuwa ilikuwa vigumu kueleza aina gani ya ulinzi ilikuwa ikihitajika kuzuia Shambulio hilo.

Ripoti hii mpya inakinzana na ripoti za awali zilizotolewa na Maafisa wa Ikulu ya Marekani ambayo ilisema kuwa shambulio hilo lililotokea likihusishwa na kupingwa kwa filamu iliyodhihaki uislam