Uganda

Watu 15 wafariki kwa ajali nchini Uganda.

Mashuhuda na polisi wakiangalia namna ya kuoka majeruhi wa ajali .
Mashuhuda na polisi wakiangalia namna ya kuoka majeruhi wa ajali . article.wn.com

Takriban watu 15 wameuwawa nchini Uganda jana Jumamosi baada ya lori liliokuwa limebeba watu takribani 40 kupinduka Mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Afisa wa polisi Ramadhan Aliga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba watu saba walifariki papo hapo huku wengine nane walifariki wakati wakikimbizwa hospitalini.

Ajali hiyo ilitokea katika wilaya Jinja, kilomita 80 Mashariki mwa mji mkuu wa Kampala, wakati lori hilo lilipokuwa likiikwepa pikipiki iliyokuwa ikija mbele yake.

Kwa mujibu wa takwimu za polisi, watu 3,000 hupoteza maisha kwa ajali za barabarani kila mwaka nchini Uganda.