MISRI

Kiongozi wa kundi la Al Qaeda awataka wamisri kupigania sheria za kiislam.

Kiongozi wa kundi la Al Qaeda Ayman al Zawahiri
Kiongozi wa kundi la Al Qaeda Ayman al Zawahiri RFI

Kiongozi wa kundi la Al Qaeda Ayman al Zawahiri amewataka wa Misri kuanzisha upya harakati zao za ukombozi kwa kusisitiza sheria za kiislam, na kutoa wito kwa waislam kuwateka raia wa mataifa ya Magharibi , mtandao wa kiintelijensia wa kundi hilo umearifu.

Matangazo ya kibiashara

Katika video iliyotolewa kwenye vikao vya wanajihadi na kutafsiriwa na taasisi ya huduma ya ufuatiliaji ya Marekani, Zawahiri pia amemkosoa Rais wa Marekani Barack Obama na kumwita mwongo na kudai alikubali kushindwa nchini Iraq, Afghanistan na Afrika Kaskazini.

Zawahiri ameema kuwa vita ndo kwanza inaanza nchini Misri,na kuwataka kila mtu nchini humo kwa dhati kupiga kampeni maarufu kuchochea na kuhubiri ili kukamilisha mapinduzi ambayo yaliharibiwa, hadi wafanikishe kurejesha thamani na heshma ya nchi yao.