Pata taarifa kuu
DR CONGO

Marekani yataka uchunguzi dhidi ya jaribio la kumuua daktari Denis Mukwege.

Msemaji wa mambo ya nje wa Marekani Victoria Nuland
Msemaji wa mambo ya nje wa Marekani Victoria Nuland thenewstribe.com
Ujumbe kutoka: Sabina Chrispine Nabigambo
1 Dakika

Marekani imeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kufanya uchunguzi wa jaribio lililofanywa la kutaka kumuua daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake hasa wale ambao wamebakwa Denis Mukwege. 

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Victoria Nuland ametoa kauli hiyo ya serikali ya Washington kuitaka Kinshasa kufanya uchunguzi kubaini ni kwa nini jaribio hilo lilifanywa.

Nuland amesema wanataka kupata taarifa ya uchunguzi hiyo kutokana na daktari Mukwege kuwa ni zaidi ya mtaalam wa masuala ya wanawake kwa kuwa amekuwa mstari wa mbele kwenye juhudi za kurejesha amani huko Bukavu.

Daktari Mukwege ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni nchini Sweden amesema nia yake ni kuhakikisha anarejea nyumbani mapema iwezekanavyo ili aweze kuendelea na shughuli zake kwenye kituo chake cha afya.

Kabla ya kuomba hifadhi ya ukimbizi nchini Sweden daktari Mukwege alinusurika kuuawa na watu wenye silaha ambao walimuua mlinzi wake mwezi Oktoba tukio ambalo linatajwa lilipangwa kutokana na yeye kuwa kinara wa kupinga ubakaji.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.