SYRIA-LEBANON

Papa Benedicto ataka amani Syria , atuma ujumbe Lebanoni.

Papa Benedicto wa XVI akiwa na rais wa Jamhuri ya Czech
Papa Benedicto wa XVI akiwa na rais wa Jamhuri ya Czech (Photo : Reuters)

Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki duniani Papa Benedicto wa XVI ametoa wito wa kusitisha machafuko nchini Syria ingawa amekiri kuwa ziara ya ujumbe wa Vatikan kwenda nchini humo iliyopangwa kufanyika hivi karibuni imeahirishwa kutokana na hali ilivyo nchini humo. 

Matangazo ya kibiashara

Papa Benedict amesema kuwa hali ya usalama nchini Syria hairuhusu endelea kwa ziara hiyo na kuongeza kuwa badala yake amemtuma mjumbe kutoka Vatican, Kadinali Robert Sarah kwenda nchini Lebanon kujadili mzozo huo.

Wakati hayo yakijiri ,Baraza la taifa la upinzani nchini humo limebainisha kuwa na matumaini kuwa suala la mzozo wa Syria litapewa kipaumbele katika ajenda za Marekani,kufuatia ushindi wa awamu nyingine wa rais Barrack Obama.

Uhusiano baina ya serikali ya rais Barrack Obama na Baraza upinzani la Syria umeongezeka zaidi kwa siku za karibuni, kwa lengo la kutafuta kuwa msemaji baina ya jumuiya ya kimataifa na vikosi vinavyopinga utawala wa rais Assad.