MALI

Wakuu wa majeshi wa ECOWAS wapitisha mpango wa kuvamia kijeshi nchini Mali

Wakuu wa majeshi wa ECOWAS
Wakuu wa majeshi wa ECOWAS france24.com

Viongozi wakuu wa majeshi wa jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS wamepitisha mpango wa kijeshi wa kuwaondoa waislam wenye msimamo mkali kutoka katika eneo la Kaskazini mwa Mali, ambako wamekuwa wakiishi kwa miezi saba sasa. 

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi mkuu wa majeshi ya Mali Ibrahim Dembele amesema kuwa wameridhishwa na mpango huo ambao uliandaliwa na wataalamu wa kimataifa ambapo vikosi rafiki vitaingia nchini Mali kupambana na waislam hao wenye msimamo mkali.

Mpango huo muhimu unataraji kupitishwa rasmi na wakuuwa nchi za jumuiya hiyo kabla ya kupelekwa mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa mnamo Novemba 26 amesema kiongozi huyo wakati wa kumalizika kwa mkutano wao huko Bamako.

Umoja wa Mataifa unataka ufafanuzi kuhusu muundo wa majeshi hayo, kiwango cha ushiriki wa mataifa mbalimbali ya Afrika magharibi pamoja na fedha za kufadhili oparesheni hiyo na mbinu za kijeshi zitakazotumika kutekeleza mpango huo.