GUATEMALA

Idadi ya waliopoteza maisha Guatemala yaongezeka

Idadi ya watu walipoteza maisha nchini Guatemala baada ya taifa hilo kupigwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha ritcher saba nukta nne imefikia watu hamsini na wawili na wengine maelfu wakikosa makazi. 

Kikosi cha waokozi wakifanya kazi usiku kucha.
Kikosi cha waokozi wakifanya kazi usiku kucha. g csmonitor.com
Matangazo ya kibiashara

Waokoaji wanaendelea kusaka miili ya watu wengine ishirini na wawili ambao hawajulikani walipo lakini wamekata tamaa ya kuwapata wakiwa hai kutokana na ugumu wanaokabiliana nao kufika maeneo yaliyoathirika kutokana na miundombinu kuharibika.

Tetemeko hilo la ardhi limesababisha uharibifu mkubwa lakini rais Otto Perez amesema wameanza kurejesha huduma ya umeme kwa asilimia tisini na tano ya nyumba zilizo kwenye eneo lililokumbwa na madhara hayo.

Marekani imetoa msaada wa dola elfu hamsini kwa waathirika wa tetemeko hilo, na kutangaza kuwa huo ni msaada katika hali ya dharura iliyowakumba na kwamba tayari wameandaa helkopta zilizo tayari kuwasafirisha.