MAREKANI

Serikali ya Marekani yatangaza kuanza uchunguzi dhidi kashfa ya ngono

O ex-diretor da CIA (agência de inteligência americana)
O ex-diretor da CIA (agência de inteligência americana) REUTERS/Yuri Gripas/Files

Serikali ya Marekani imetangaza kuanza uchunguzi dhidi ya Mkuu wa Vikosi Vinavyolinda Amani nchini Afghanistan chini ya mwamvuli wa NATO, ISAF Jenerali John Allen ambaye amehusishwa kwenye kashfa ya mapenzi inayomkabili pia aliyekuwa Mkuu wa CIA David Petraeus

Matangazo ya kibiashara

.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Leon Panetta ametangaza kufanyika kwa uchunguzi huo kubaini kama Jenerali Allen amehusika kwenye sakata hilo la mapenzi linalojumuisha kutumiana barua pepe.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi wa Marekani George Little ndiye ambaye ametangaza kuanza kwa uchunguzi huo huku akisistiza Jenerali Allen ataendelea na wadhifa wake kama ilivyokuwa awali.

Kuibuka kwa kashfa hii ya ngono ambayo imewagusa Viongozi wa Juu kwenye vyombo vya usalama nchini Marekani imeonekana kuchafua utendaji wao na hivyo wanaamini kuna kazi kubwa ya kuwasafisha.

Aliyekuwa Mkuu wa CIA David Petraeus binafsi tayari alishakiri kuhusika na kashfa ya mapenzi nje ya ndoa na kuchukua hatua ya kujiuzulu wadhifa wake.