RWANDA-DRC-UN

Rwanda yaituhumu DRC kuishambulia kwa makombora

Baadhi ya Waasi wa kundi la M23 ambao wanaaminika kuukaribia mji wa Goma na kutishia usalama wa mji huo
Baadhi ya Waasi wa kundi la M23 ambao wanaaminika kuukaribia mji wa Goma na kutishia usalama wa mji huo REUTERS/James Akena

Makabiliano yameendelea kushuhudiwa kati ya waasi wa kundi la M23 na vikosi vya serikali ya Congo FARDC karibu na mji wa Goma, mashariki mwa jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakati mvutano ukiibuka ambapo Rwanda inashutumu majeshi ya Congo kuishambulia kwa makombora, jambo ambalo linakanushwa vikali na serikali ya Kinshasa.

Matangazo ya kibiashara

Hapo jana waasi wa M23 waliipa serikali ya Congo muda wa saa 24 kuanzisha mazungumzo na kuondolewa kwa wanajeshi wake katika mji wa Goma, jambo ambalo lilitupiliwa mbali na serikali ya rais Kabila ikidai kuwa hawawezi kuzungumza na M23 kwakuwa Rwanda ndio ambayo inawashambulia, hivyo waasi wa m23 wakaanzisha mashambulizi.

Kanali Oliver Hamuli amezungumzia Rwanda ilivyoshambulia kwa moto DR Congo na kusababisha majeraha kwa askari katika kipindi cha hivi karibuni.

Kwa mujibu wa mashuhuda mashambulizi yalijiri katika upande wa kaskazini na kaskazini magharibi mwa Goma na kusababisha wakazi kuyakimbia makazi yao kuelekea kusini na wengine kwenye mpaka wa Rwanda.

Duru za kitabibu zinaarifu kuwa watu zaidi ya ishirini walipelekwa hospitalini baada ya kujeruhiwa ambapo mmoja alipoteza maisha, na hadi sasa hakuna idadi nyingine ambayo imekwisha tolewa.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwaondoa wafanyakazi wake wasiokuwa na kazi kubwa, huku wanajeshi wakisalia jijini Goma kukamilisha jukumu lao la kuwalinda wananchi.