DRCongo-mapigano

Waasi wa M23 waendelea kuiteka miji kadhaa licha ya kutakiwa waondoke mjini Goma

Goma, Novemba 21, mwaka 2012
Goma, Novemba 21, mwaka 2012 AFP PHOTO/Tony KARUMBA

Waasi wa M23 ambao wameuteka mji wa Goma na Sake Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokarsia ya Congo sasa wanasema kuwa wanalenga kuteka miji zaidi kama Bukavu, Kisangani na Kinshasa. Jijini Kampala Uganda marais Joseph Kabila,Paul Kagame wa Rwanda na mwenyeji wao Yoweri Museveni wameafikiana kuwa ni sharti waasi hao waondoke katika mji wa Goma huku rais Kabila akisema yuko tarayio kuzngumza na waasi hao.

Matangazo ya kibiashara

Askari wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC), ambao siku moja kabla walipiga kambi yao mjini Sake, wameuacha mji huo na kuelekea kusini muda mfupi kabla ya waasi wa kundi la M23

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Augustin Matata Ponyo ambaye, baada ya kuishutumu nchi ya Rwanda kusaidia waasi wa M23, alieleza kuwa serikali yake iko pamoja na wananchi wa mkoa wa Kivu Kaskazini na kusema kwamba  bado upo uwezekano wa kupata suluhu.

Hata hivyo, wabunge na maseneta nchini humo wanashangazwa na ukimya wa Rais Kabila kama Amiri Jeshi na wengine kufikia hata kuomba rais huyo ajiuzulu. mwenyekiti wa chama cha upinzani cha FONUS Joseph Olengankoy amemtaka rais Kabila kujiuzulu kwa kusihdnwa kuwalinda raia wake.

hapo jana yameshuhudiwa maandamo ya raia katika miji ya Bunia na Bukavu, wananchi wakionyesha hasira yao kufwatia kutekwa kwa mji wa Goma na kundi la waasi wa M23. Ofisi za shirika la Umoja wa Mataifa nchini Jamuhuri y kidemokrasia ya Congo MONUSCO na za chama Twala PPRD zililengwa na waandamanaji.

Wakati huo huo Umoja wa wanafunzi kutoka nchini jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wanaosoma nchini Rwanda wanasema wamesikitshwa na rais Joseph Kabila kushindwa kuwazuia waasi wa M 23 kuuteka mji wa Goma na sasa ule wa Sake.