PALESTINA-UN

Umoja wa Mataifa wapitisha azimio kuhusu uanachama wa Palestina , wapalestina washerehekea hatua hiyo

REUTERS/Mohamad Torokman

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ameshukuru mataifa ambayo yamewaunga mkono kwenye azimio lao la kutaka kupata uanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa UN licha ya kukutana na upinzani kutoka kwa Israeli na Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN umepiga kura ya kuiwezesha Mamlaka ya Palestina kupata uanachama rasmi wa Umoja huo baada ya kuwasilisha pendekezo lao na tayari wananchi wa Taifa hilo wanasherehekea ushindi huo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon amesema anaamini Wapalestina wanahaki ya kupata uanachama rasmi wa Umoja huo na hivyo ni kitu kizuri kupata uungwaji mkono.

Kwa upande wake Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa UN Susan Rice ameendelea kushikilia msimamo wa nchi yake kupinga hatua hiyo na kuweka bayana ilikuwa bahati mbaya kwao kushinda.

Nchi wanachama mia moja thelathini na nane zimepiga kura ya kuunga mkono hatua ya Mamlaka ya Palestina kupata uanachama rasmi huku tisa zikipiga kura ya hapana na nyingine arobaini na moja zikikataa kupiga kura.

Hatua inaangaliwa na wachambuzi wa mambo kama hatua ambayo inaweza ikazua mgogoro zaidi baina ya Palestina na Israeli kwa kuwa Israeli haikubaliani na kile kilichotokea.