LONDON

Benki ya Uingereza ya HSBC kuilipa Marekani Dola Bilioni 1 nukta 9

Benki ya HSBC yenye makao yake nchini Uingereza imethibtisha kuwa itailipa serikali ya Marekani Dola Bilioni 1 nukta 9, baada ya ushahidi kubainisha kuwa imekuwa ikitumiwa katika biashara ya ulanguzi wa fedha.

Matangazo ya kibiashara

Marekani imekuwa ikiituhumu benki hiyo kuwasaidia wafanyibiashara wanaojishughulisha na biashara ya fedha kutumia huduma zake pamoja na wale wanaouza dawa za kulevya.

Mwezi uliopita, Benki ilitangaza kuwa imetenga Dola Bilioni 1 nukta 5 kulipa faini zozote ambazo zingejitokeza dhidi ya taasisi hiyo ya fedha .

Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Stuart Gulliver amesema wanakiri makosa waliyoyafanya na wanaajibika vilivyo.

Uongozi wa Benki hiyo unasema umetumia Dola Milioni 290 kupambana na biashara haramu ya fedha kwa kukarabati mitambo ya kusaidia kupunguza biashara hiyo haramu.

Uchunguzi wa wabunge wa Senate nchini Marekani umebaini kuwa Akauti za Benki hiyo ya HSBC zimekuwa zikitumiwa na walanguzi wa dawa za kulevya nchini Marekani na Mexico.

Benki ya HSBC inasalia kuwa benki kubwa barani Ulaya kutoa huduma za kifedha.