VENEZUELA-CUBA

Rais Chavez akabiliwa na maradhi mengine akiendelea kupatiwa tiba nchini Cuba na hali yake mbaya

Wananchi wa Venezuela wakiwa wanagusa picha ya Rais Hugo Chavez wakimuombea kipindi hiki afya yake ikizidi kuzorota nchini Cuba
Wananchi wa Venezuela wakiwa wanagusa picha ya Rais Hugo Chavez wakimuombea kipindi hiki afya yake ikizidi kuzorota nchini Cuba REUTERS/Jorge Silva

Rais wa Venezuela Hugo Chavez ambaye amerejea nchini mwake baada ya kupatiwa matibabu nchini Cuba kutokana na kukabiliwa na saratani pamoja na mfumo wake wa upumuaji hali yake imeanza kuwa mbaya kutokana na kusumbuliwa na maradhi mengine.

Matangazo ya kibiashara

Rais Chavez hali yake inatajwa kuwa mbaya kutokana na kupata maradhi mengine tofauti na yale ambayo yamebainika awali nchini Cuba kitu ambacho kimeanza kuzua hofu juu ya hali yake katika siku za baadaye.

Makamu wa Rais Nicolas Maduro ameliambia Taifa kupitia Radio na Televisheni hali ya afya ya Rais Chavez ni mbaya kutokana na kuanza kusumbuliwa na maradhi mengine ambayo bado hayajabainika na Madaktari.

Rais Chavez ambaye bado hajaapishwa tangu ashinde kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu kilichofanyika mwezi Novemba mwaka huu anakabiliwa na ugonjwa wenye utata kitu ambacho kimerejea hofu kubwa kwa wafuasi wake.

Makamu wa Rais Maduro amekiri kuzungumza na Rais Chavez na kusema anapitia kwenye kipindi kigumu kwa sasa kutokana na kukamatwa na maradhi hayo ambayo yamefanya afya yake izorote kwa kiasi kikubwa.

Maduro licha ya kueleza hali ya afya ya Rais Chavez lakini amewaambia wananchi Kiongozi wao anawatakiwa kila la kheri katika kumaliza mwaka na kuelekea mwaka mpya na kuzidi kumuombea aweze kurejea katika hali yake ya awali.

Makamu wa Rais akiwa Havana amesema ataendelea kuwepo nchini Cuba kwa siku kadhaa kabla ya kurejea Venezuela lengo likiwa ni kukaa karibu na familia ambayo inapitia kipindi kigumu kutokana na Kiongozi wao kuendelea kuugua.