PAKISTAN-AFGHANISTAN-MAREKANI

Mashambulizi ya angani ya Wanajeshi wa Marekani yasababisha kifo cha Kamanda wa Taliban, Mullah Nazir

Kamanda wa Kundi la Wanamgambo wa Taliban Mullah Nazir ambaye ameuawa kwenye mashambulizi ya angani nchini Marekani
Kamanda wa Kundi la Wanamgambo wa Taliban Mullah Nazir ambaye ameuawa kwenye mashambulizi ya angani nchini Marekani

Mashambulizi ya angani yaliyofanywa na Wanajeshi wa Marekani nchini Pakistani yamesababisha kifo cha Mbabe wa Kivita na Kamanda wa Kundi la Wanamgambo la Taliban Mullah Nazir. Mashambulizi hayo ya angani yametekelezwa katika eneo la Kaskazini Magharibi mwa Pakistan na kusababisha vifo vya wapiganaji wengine tisa wa Kundi la Taliban taarifa za kiusalama zimethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Nazir ni Kamanda wa Kundi la Taliban ambaye anatajwa kupeleka wapiganaji nchini Afghanistan kwa lengo la kupambana na Vikosi vya Kujihami vya Nchi za Magharibi NATO ambavyo vinashika doria katika Taifa hilo.

Kamanda Nazir alikuwa Kiongozi wa Taliban katika eneo la Kusini mwa Waziristan ukanda ambao unatajwa kuwa na wapiganaji wengi wenye uhusiano na Mtandao wa Kigaidi Duniani Al Qaeda.

Maofisa wa Serikali ya Pakistan wamesema Nazir ameuwa kwenye mashambulizi mawili ya angani ambayo yalitekelezwa kulenga gari lake katika eneo la Birmil ambapo watu watano wa familia yake walipoteza maisha.

Pakistan imethibitisha licha ya wanafamilia watano wa Nazir kupoteza maisha lakini pia wasaidia wake wawili ni miongoni mwa wale waliopoteza maisha kwenye mashambulizi hayo ya angani huko Waziristan.

Nazir alifikia makubaliano na Islamabad mwaka 2007 juu ya mpango wa amani na kuanza kuwa na mahusiano mazuri na Pakistan hasa Kundi la Taliban ambalo lilikuwa linapambana kwa ajili ya maslahi yao.

Hofu imeanza kutanda nchini Pakistan huenda Kundi la Wanamgambo la Taliban likafanya mashambulizi ya kulipiza kisasi kutokana na kifo cha Kamanda Nazir ambaye alikuwa nguzo muhimu kwa kundi hilo huko Islamabad.