Venezuela

Maandamano ya Upinzani Venezuela kufanyika iwapo Rais Chavez hatasimama kuapishwa

Rais wa Venezuela, Hugo Chavez
Rais wa Venezuela, Hugo Chavez

Kiongozi wa upinzani wa juu nchini Venezuela, ameitisha maandamano ikiwa Serikali ya nchi hiyo itachelewesha shughuli za kuapishwa kwa Rais wa Taifa hilo Hugo Chavez ambaye hali yake yaelezwa kukutereka baada ya kufanyiwa upasuaji kwa awamu ya nne.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa Upinzani Julio Borges pia ameahidi kufungua kesi ya malalamiko ikiwa tarehe 10 ya mwezi Januari iliyopangwa kuapishwa kwa Rais haitatekelezwa.
 

Upinzani umedai kuwa Mamlaka ya Venezuela inapindisha katiba kutokana na matatizo ya ndani ya nchi
 

Upinzani umefikia hatua hiyo imefikiwa wakati kukiwa na taarifa kuwa huenda Cahvez asiapishwe siku ya Alhamisi kufuatia hali yake kuwa tete.
 

Upinzani umesema kuwa muda wa kuhudumu kwa Chavez unakoma siku ya Alhamisi ya juma hili ikiwa hatajitokeza kwa ajili ya kuapishwa hivyo Speaker wa Bunge atachukua madaraka ya Uongozi badala yake.
 

Chavez alichaguliwa tena katika kipindi cha awamu ya sita mwezi 0ctoba mwaka jana licha ya ugonjwa wa Saratani unaomkabili.