Tunisia-Maandamano

Maandamano zaidi nchini Tunisia ya kupinga mauaji ya kiongozi wa upinzani Chokri Belaid

Polisi nchini Tunisia imetumia bomu za kutowa machozi kwa kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamekusanyika kwa wingi wakivamia kwenye makao makuu ya polisi jijini Sidi Bouzid kitovu cha harakati za maandamano, wakipinga mauaji ya kiongozi mkuu wa upinzani Chokri Belaid.

Gari za kusafirishia wagonjwa ikiubeba muili wa  Chokri Belaïd, kiongozi mkuu wa upinzani alieuawa Februari 6
Gari za kusafirishia wagonjwa ikiubeba muili wa Chokri Belaïd, kiongozi mkuu wa upinzani alieuawa Februari 6 Reuters / Souissi
Matangazo ya kibiashara

Takriban waandamanaji mia hivi walivamia kituo cha polisi jumatano hii ambapo polisi ililazimika kutumia bomu za kutowa machozi ili kuwatawanya watu hao. Jeshi liliazimika kuingilia kati ili kutuliza ghasia hizo.

Wakati huo waandamani wanaokadiriwa kufikia elfu mbili wameandamana katika hali tulivu jijini Sidi Bouzid ambako mfanyabiashara wa barabarani alianzisha maandamano mwaka 2010 yaliomg'oa rais Zine El Abidine Ben Ali madarakani.

Majengo ya ofisi za chama cha Ennahda madarakani, yalishambuliwa katika eneo tatu tofauti, wakati wafuasi wa kiongozi wa upinzani Chokri Belaid alieuawa wakikituhumu chama hicho kuhusika na mauaji hayo.

Mamia ya waaandamanaji walivamia ofisi za chama madarakani cha Ennahda katika mji wa Mezzouna uliopo kwenye umbali wa kilometa 75 kusini mashariki mwa mji wa Sidi Bouzid kabla ya kuyateketeza kwa moto.

Mjini Gafsa, waandamanji wameshambulia ofisi za chama madarakani cha Ennahda na kuvunja meza na viti vyote vya ofisini na kuchana mabago yote ya chama hicho na baadae kuondoka na vifaa vya ofisini kama vile compyuta na vifaa vingine na kwenda kuviteketeza kwa moto barabarani.

Mashahidi wanasema kuwa ofisi za chama hicho katika mji wa Kef kaskazini mashariki, yalishambuliwa na waandamanaji wenye hasira.

Katika mji wa Kasserine, shughuli za masomo zili sitishwa na wandamanaji wakusanyika kwa wingi huku waki lalamika”kisase, kisase, kisake” katika mji huo uliokaribu na mpaka na Algeria.

Maandamano pia yameshuhudiwa katika miji mingine nchini humo hususan katika mji mkuu Tunis ambapo watu wanaokadiriwa kufikia elfu 4 walikusanyika katika ofisi za wizara ya mambo ya ndani wakitowa maneno y kuilani serikali.