Côte d’Ivoire-Ufaransa

Maharamia walioiteka meli ya Ufaransa iliokuwa ikielekea nchini Côte d’Ivoire waiachia huru

Meli ya mafuta ya Ufaransa iliyokuwa imetekwa na maharamia wakati ikielekea nchini Cote D' Ivoire siku ya jumapili juma lililopita imeachiwa na maharamia hao.Emmanueli Mmbando ana taarifa zaidi

Meli ya Ufaransa iliokuwa imetekwa na maharamia
Meli ya Ufaransa iliokuwa imetekwa na maharamia
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo hakuna taarifa rasmi zinazoeleza sababu za kuachiwa kwa meli hiyo pamoja na watu 17 waliokuwa ndali ya meli huku watu wawili kati ya hao wanaendelea na matibabu baada ya kujeruhiwa wakati wa utekaji.

Aidha bado haijajulikana kitu kilichowashawishi maharamia hao na hata kuichilia huru meli hiyo iliyokuwa na wafanyakazi wenye asili ya Afrika na Asia.

Matukio ya mashambulizi yanayofanywa na maharamia na utekaji nyara wa meli katika miaka ya hivi karibuni yameoongezeka katika ukanda wa nchi za Afrika Magharibi huku lengo likiwa ni kupora fedha na wizi wa mafuta.

Mwezi uliopita maharamia wenye silaha waliichia meli ya mafuta ya Nigeria waliyokuwa wameiteka huko Cote D' Ivoire baada ya kufanikiwa kutoroka na mafuta yenye thamani ya dola milioni tano.

Matukio hayo yanatokea huku jitihada mbalimbali zikifanywa na jumuiya kimataifa kupamba na vitendo vya utekaji vinavyofanywa na maharamia katika nchi mbalimbali duniani.