Marekani-Yemeni

Shirika la kijasusi la CIA lagundulika kuendesha mashambulizi bila idhini ya viongozi wa Yemeni

Ndege za Marekani zisizokuw ana rubani Drone
Ndege za Marekani zisizokuw ana rubani Drone

Shirika la kijasusi la Marekani CIA limegundulika kuwa limekuwa likifanya operesheni za kijeshi kwa siri nchini Saudi Arabia kwa miaka miwili iliyopita kwa kutumia ndege zisizo na rubani.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa zilizoibuliwa na vyombo vya habari nchini Marekani zinasema kuwa Marekani ilifanya hivyo kwa ajili ya kuwawinda wanachama wa kundi la Al-Qaeda katika maeneo ya Penisula ya Uarabuni iliyo chini ya nchi ya Yemeni kama harakati za kukomesha vitendo vya kigaidi.

Hata hivyo Marekani inadaiwa kuendesha operesheni hiyo ya kijeshi bila idhini ya nchi ya Yemeni vimebainisha vyombo vya habari nchini Marekani.

Ndege isiyo na rubani iliyorushwa kutoka katika eneo hilo ilitumika kumuua Anwar al-Awlaki kiongozi wa kidini aliyekuwa anatuhumiwa kuwa mkuu wa operesheni za nje za Al- Qaeda mwezi septemba mwaka 2011.

Hata hivyo vyombo vya habari nchini Marekani vidaiwa kuwa vilifahamu taarifa za operesheni hiyo ya marekani miaka miwili iliyopita lakini havikutangaza na kuchapisha habari hizo hali inayoibua maswali mengi.

Marekani iliondoa vikosi vyake vyote nchini Saudi Arabia mwaka 2003 baada ya kumalizika kwa vita vya mwaka 1991 na kubakiza kikosi cha kutoa mafunzo pekee.