Misri-Syria

Viongozi wa ulimwengu wa Kiislam wakutana jijini Cairo kwa ajili ya kujadili suala la Syria na Mali

Viongozi wa ulimwengu wa kiislam wanakutana jijini Cairo nchini Misri ambapo mzozo wa Syria uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili sasa na uingiliaji kijeshi wa mzozo wa Mali ni mambo ambayo yatagubikwa mkutano huo. Viongozi hao katika mkutano huo unaozinduliwa leo mchana, watatowa wito kwa mazungumzo ya kweli baina ya upinzani na wawakilishi wa serikali ya rais Bashar Al Assad ambayo ipo tayari kwa mabadiliko ya kisiasa katika mapendekezo yaliotolewa na mawaziri wa nchi za nje wa Jumuiya ya nchi za kiarabu.

Waziri wa mambo ya nje wa Misri Mohamed Kamel Amr na katibu mkuu wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu Ekmeleddin Ihsanoglu
Waziri wa mambo ya nje wa Misri Mohamed Kamel Amr na katibu mkuu wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu Ekmeleddin Ihsanoglu
Matangazo ya kibiashara

Muswada huo uliwasilishwa na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 56 wanachama wa Jumuiya ka Kiislam waliokutana Jumatatu na jumanne jijini Cairo unaoagiza mazungumzo yatayofikia katika makubaliano ya uwepo wa kipindi cha mpito katika kuzingati matakwa ya wananchi wa Syria ya mabadiliko ya kidemokrasia na mabadiliko ya utawala.

Licha ya kuheshima mipaka ya taifa la Syria, muswada huo, unatafisir kuwa serikali ya Syria ndio muhusika wa kwanza wa mauaji ya watu elfu sitini waliouawa katika kipindi cha miaka miwili.

Hata hivyo katika muswada huu mawaziri hawakuweka bayana hatma ya rais Bashar Al Assad ambae upinzani unamtaka kuondoka madarakani lakini pia nchi za Saudia Arabia na Qatar.

Uwepo wa rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad katika mkutano huo ambae ni mshirika wa karibu na utawala wa Syria na ambae amekuwa akipinga pendekezo kuondolewa madarakani rais Bashar Al Assad kama njia ya kufikia muafaka, huenda mkutano huo ukakwamisha mkutano huo unaoongozwa na rais wa Misri Mohamed Morsi.

Upinzani nchini Syria waonekana kugawanyika ambapo baraza la kitaifa nchini humo lilitupilia mbali pendekezo la mazungumzo na serikali ya Damascus baada ya kiongozi wa muungano wa upinzani Ahmed Moaz al Khatib ambae anaungwa mkono na Jumuiya ya nchi za kiarabu pamoja na Marekani kudai kuwa tayari kwa mazungumzo na serikali ya rais Bashar al Assad.

Mbali na Syria viongozi wa Jumuiya ya nchi za kirabu watajadili kuhusu mzozo wa Mali ambao uliwafanya viongozi wa nchihiyo kugawanyika kuhusiana na uingiliaji kijeshi na Ufransa huko kaskazini mwa Mali ambapo nchi kama vile Misri na Qatar zilitangaza kupinga uingiliajihuo kijeshi na kuomba mazungumzo