Mali-Ufaransa

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian akiri majeshi yake kupata upinzani mkali jijini Gao

Majeshi ya Ufaransa yaliopo nchi Mali tangu Januari 11, mbali na kuripotiwa kifo cha mwanajeshi mmoja, hapo jana yamekutana na upinzani mkali baada ya kukabiliana na mashambulizi ya makundi ya kiislam katika mji wa Gao. Wanashi kadhaa wamejeruhi katika makabiliano hayo, amethibitisha waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian bila hata hivo kutaja idadi.

Vikosi vya Ufaransa nchini Mali
Vikosi vya Ufaransa nchini Mali
Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo amesema majaeshi yake yamepambana vikali na kuna wanajeshi kadhaa waliojeruhiwa, na kutangaza maskitiko ya kifo cha mtu mmoja. Hata hivo waziri huyo hakusema ni katika mazingira gani ya kifo cha mwanajeshi huyo na idadi ya waliojeruhiwa na lini yalitokea mashambulizii hayo.

Waziri Le Drian amesema ndege za kijeshi zinajaribu kuendesha mashambulizi katika ngome za wapiganaji wa makundi ya kiislam na kushambulia gari za wapiganaji hao, hivyo kuwepo na vita vya ukwelikatika mji wa Gao.

Kundi la Vuguvugu kwa ajili ya muungano wa jihadi Afrika Magharibi (Mujao) lilokuwa likiushikilia mji wa Gao limejigamba jana jioni kushambulia kwa roketi ngome ya wanajeshi wa Ufaransa na wa Afrika jijini Gao.

Duru kutoka ngome ya majeshi ya Afrika magharibi nchini Mali (Misma) ambapo takriban wanajeshi mia mbili wapo kwenye uwanja wa mapambano Zimekanusha taarifa ya kushambuliwa kwa ngome ya jijini Gao.

Le Drian amesema kwamba tangu kuanza kwa mashambulizi ya kijeshi nchini Mali Januari 11, kuna majeruhi kadhaa wa kawaida upande wa majeshi ya Ufaransa mbali na kifo cha rubani alieuawa mwanzoni mwa operesheni hiyo.

Jumla ya wanajeshi elfu nne kutoka Ufaransa wanapatikana nchini Mali ambapo ni mara mbili ya idadi iliokuwa imefahamishwa mwanzoni mwa Operesheni jiyo ya vikosi vya Ufaransa nchini Mali, vikilingana na idadi ya wanajeshi wa Ufaransa vilivyotumwa nchini Afghanistani mwaka 2010 na havitoognezwa kwa mujibu wa waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian.

Upande wa wapiganaji wa kiislam wamepata pigo kubwa ingawaje waziri wa uliinzi wa Ufaransa alikataa kutowa idadi, lakini wizara yake imesema ma mia ya wapiganaji waliuawa katika mashambulizi ya anga ya ndege za Ufaransa wakati walipokuwa katika magari yaliokuwa yakiwabeba wapiganaji na silaha na kwenye mapambano ya ana kwa ana katika mji wa Kanna na Gao