Mali-Ufaransa

Ufaransa yaomba kutumwa kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Mali

Balozi wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Gerard Araud
Balozi wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Gerard Araud

Ufaransa imeliomba baraza la Uslama la Umoja wa Mataifa kuandaa kutumwa vikosi vya Umoja huo nchini Mali. Vikosi hivyo vitatumwa nchini Mali punde wakati operesheni za kijeshi zitapokamilika, mwezi Machi au Aprili mwaka huu. Wakati huo huo balozi wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Gérard Araud ameutaka Umoja wa Mataifa kuwatuma mara moja waangalizi wa haki za binadamu nchini Mali katika miji iliokuwa ikikaliwa na wapiganaji wa makundi ya kiislam, ili kuepusha vitendo vya ulipizaji kisase ambavyo vinaweza kuzuka hapo baadae.

Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha kijeshi cha Umoja wa Afrika (Misma) ambacho uundwaji wake umechukuwa muda mrefu, kwa sasa kimewekwa kando, na badala yake kikosi cha Umoja wa Mataifa ndicho kitachotumwa huko Mali, ambapo wanajeshi wa Afrika ambao tayari wapo huko nchini Mali Balozi Araud amesema watajiunga na kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa.

Balozi Gerard Araud amenukuliwa akisema kwamba: Ukweli ni kwamba iwapo nchi zitataka kuweka vikosi vya Misma chini ya Umoja wa Mataifa, labda kutakuwa vikosi vingine, na huenda vingine vitakataa kujiunga, haitakuwa vikosi viwili tofauti, bali kikosi cha Umoja wa Mataifa kikiongozwa moja kwa moja na baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama ilivyo kwa vikosi vyote vya Umoja huo.

Uongozi huo wa vikosi vya kijeshi na Umoja wa Mataifa unachukuliwa kama wenye nguvu zaidi na rahisi kuongoza badala yakuwa na uongozi kutoka Umoja wa Afrika na Ecowas, na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa watakusanyika kaskazini mwa Mali.

Uwepo wa vikosi vya Umoja wa Mataifa kusini mwa Mali bado wajadiliwa. Baadhi ya wanajeshi wa mapinduzi ya kijeshi jijini Bamako bado wanasitasita kukubali ujio wa vikosi hivyo kusini mwa Mali