Tunisia-Mazishi

Mamia ya wananchi wajitokeza nchini Tunisia kushiriki mazishi ya kiongozi wa upinzani Chokri Belaid

Mazishi ya kiongozi wa upinzani Chokri Belaïd, tarehe  8 Februari 2013
Mazishi ya kiongozi wa upinzani Chokri Belaïd, tarehe 8 Februari 2013 REUTERS/Anis Mili

Halaiki ya watu wamejitokeza nchini Tunisia kuhudhiria mazishi ya kiongozi mkuu wa upinzani Chokri Belaid aliyeuawa juzi jumatano akiwa nje kidogo ya nyumbani kwake jijini Tunis. Shughuli za usafiri wa ndege zimesitishwa, huku kukiwa hakuna usafiri kama ilivyo kawaidfa kufuatia mgomo uliotishwa na chama kikuu cha wafanyakazi nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Mamia ya watu wamejitokeza kuhudhuria mazishi ya kiongozi huyo aliauawa wakati alipokuwa akitoka nyumbani kwake na kukutana na mtu ambae alimlenga na kumpiga risasi tatu kifuani na kufariki papo hapo, hali ambayo ilizua hasira na ghadhabu miongoni mwa wananchi waliteremka barabarani wakiandamana na wengine wakiteketeza makao makuu ya chama tawala cha Ennahda.

Wananchi waliokuwa kwenye msafara wa kuelekea kwenye safari ya mwisho ya kiongozi huyo wa upinzani walionekana wenye huzuni na hasira huku wakitokwa na maneno ya kukikashifu chama tawala, huku wakimtuhumu kiongozi mkuu wa chama kilichopo madarakani Ghannouchi kuwa ni muuaji, na wengine wakidai kuwa wananchi wanahitaji mabadiliko.

Wengi wa waliosindikiza jeneza la Chokri Belaid wamesema wamesikishwa na kifo cha kiongozi huyo ambae wamesema alikuwa mtetezi wa wanyonge na aliauwa kwa sababu alikuwa akitetea watu masikini. Mama mmoja alisikika akisema huku akilia kwamba watu kutoka vyama tofauti ambao wanashiriki mazishi ya kiongozi huyo ni watu ambao wanataka kuwa na fikra huru kama alvyokuwa Chokri

Wanasiasa kadhaa wa upinzani wameshiriki katika mazishi hayo akiwemo Beji Caïd Essebsi aliewahi kuwa wakati mmoja waziri mkuu katika kipindi cha mpito ambapo mshirika wake wa karibu Tatouine aliuawa mwezi Octoba mwaka jana.

Wengi ya wanasiasa walioshiriki katika mazishi hayo walionekana kulindwa zaidi, baada ya kupokea vitisho na vitimbi, hivyo serikali kuamuwa kuwalindia usalama zaidi na hata njia walizotumia katika kuelekea mazikoni hazikuwekwa wazi