Tunisia

Mgomo wa jumla waitishwa nchini Tunisia wakati mazishi ya Kiongozi wa upinzani Chokri Belaid yakifanyika, huku Marekani ikiwatolea wito wa kuwa watulivu

Tunis,  tarehe 7 Februari 2013.
Tunis, tarehe 7 Februari 2013. REUTERS/Louafi Larbi

Mgomo wa jumla umeitishwa nchini Tunisia wakati mazishi ya kiongozi wa upinzani Chokri Belaid alieuawa hivi majuzi yakifanyika, mauaji ambayo yalizua ghasia na hasira miongoni mwa wafuasi wa upinzani na hivo kuhatarisha hali ya kisiasa ilikuwepo nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha kiislam madarakani cha Ennahda kimetupilia mbali uamuzi wa waziri mkuu Hamadi Jabali wa kuunda baraza jipya la mawaziri lenye wajumbe wasiokuwa na mrego wowote wa kisiasa ili kutatua matatizo ya kisiasa yaliopo, wakati rais Moncef Marzouki akiunga mkono uundwaji wa serikali ya muungano.

Hata hivyo ofisi ya rais imesema haina taarifa yoyote na haijapokera barua yoyte ya kujiuzulu kwa waziri mkuu na pendekezo la majina ya mawaziri baada ya waziri mkuu kutangaza nia yake ya kuunda baraza jipya la mawziri.

Hayo yanajiri wakati shughuli za usafiri zikizorota katika mji mkuu Tunis, chama cha wafanyakazi UFTT kilitowa wito wa mgomo wakati wa mazisihi ya kiongozi wa upinzani alieuawa Chokri Belaid. Uwanja wa ndege wa Tunis unafanya kazi kama kawaida ispokuwa shguhuli za uwanja huo zimevurugwa na safari nyingi za ndege zimeahirishwa, wamethibitishwa viongozi wa shirika na denge la mjini Tunis.

Chama hicho cha umoja wa wa wafanyakazi nchini Tunisia licha ya kuitisha mgomo kimewatolea wito wa wananchi kuwa watulivu na kusema kwamba ni mgomo wa amani kulaani mauaji.

Baada ya kifo cha kiongozi wa upinzani Chokri Belaid juzi jumatano ghasia na machafuko vilizuka na kusababisha kifo cha askari polisi mmoja.
Kiongozi huyo wa upinzani anazikwa leo mjini Djebel Jelloud kusini mwa viounga vya mji mkuu Tunis.

Wakati huo huo Marekani imetaka Viongozi wa Tunisia kuungana na kuondoa hali ya machafuko yaliyokumba nchi hiyo, ikionya kuwa hakuna nafasi tena ya nchi ya Tunisia kurejea yale ambayo yalipitiwa.

Washington imekemea kitendo cha mauaji ya kiongozi wa upinzani Chokri Belaid aliyeuawa kwa Risasi siku ya jumatano nje ya nyumbani kwake mjini Tunis hali iliyosababisha maandamano makubwa nchini humo.