EU-mkutano

Viongozi wa Ulaya waendelea kulumbana kuhusu bajeti ya Umoja huo

Viongozi wa Umoja wa Ulaya katika mkutano wa Brussels
Viongozi wa Umoja wa Ulaya katika mkutano wa Brussels

Viongozi wa Umoja wa Ulaya EU wametofautiana kuhusu bajeti ya Jumuiya hiyo, kutokana na baadhi ya nchi hususan Uingereza zikitaka mpango wa kubana matumizi ya fedha huku Ufaransa na Italia zikipendekeza bajeti ilenge zaidi kuunda nafasi za kazi na kuinua uchumi. Viongizi hao wamekutana usiku kucha kupanga bajeti ya miaka kumi na Jumuiya hiyo katika makao makuu ya Umoja huo jijini Brussels Ubelgiji huku mazungumzo yakiendelea leo Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya tofauti hizo, rais wa Umoja huo Herman Van Rompuy amesema kuwa kuna matuamini ya suluhu kupatikana kuhusu bajeti hiyo inayokadiriwa kuwa Euro trilioni moja.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema kiwango cha matumizi ni kikubwa mno, na kuongexza kuwa wapo tayari kutumia kura ya turufu kukwamisha badgeti hiyo

Upande wake Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema ni mapema mono kukiri kwamba kutakuwa makubaliano kwani bado kuna mvutano baina ya pande mbili.