Iraq-Mashambulizi

watu 29 wauawa nchini Iraq katika matukio tofauti

Takriban watu 29 wameuawa na wengine zaidi ya kumi wamejeruhiwa leo siku ya Ijumaa katika matukio tofauti ya kuvizia dhidi ya waumini wa kiislam wa madhehebu ya kishia nchini Iraq.

REUTERS/Ako Rasheed
Matangazo ya kibiashara

Mashambulio ya aina hiyo yameongezeka katika kipndi cha juma moja na kusababisha vifo vya watu 100 katika kuelekea maadhimisho ya miaka 10 tangu kuvamiwa kwa iraq mwaka 2003 yaliopelekea kuanguka kwa Utawala wa Saddam Hussein ambapo vikosi vilivyo vamia nchini hiyo viliondoka mwaka 2011.

Kaskazini mwa mji mkuu Bagdad, gari mbili zililipuka katika nyakati tofauti kwenye soko la mifugo aina ya ndege mjini Kazimiya mji ambao unakaliwa na idadi kubwa ya waislam wa madhehebu ya kishia na kusababisha vifo vya watu 16 na majeruhi 43, duru za kitabibu na za kijeshi zathibitisha.

Soko hiyo hufurika watu wengi kwa kuwa ni sku ya mapumziko hivo watu wengi hutembelea katika soko hiyo.

Kusini mwa mji mkuu katika mji mwingine wenye waumini wengi wa kishia wa Babylone gari mbili zililipuka mjini shomali na kusababisha vifo vya watu 13 na wengine 26 kujeruhiwa kulingana na duru za kitabibu na za kijeshi.

Mlipuko wa kwanza ulitokea karibu na mji huo ni mwingine wapili ulitokea katika soko moja. Wanawake na watoto ni miongoni mwa wahanga.

Washambuliaji wa ki sunni hususan wale wa kundi la Alqaeda nchini Itaq wanawalenga ndugu zao wa kishia au vikosi vya usalama ili kujaribu kuyumbisha usalama wa serikali inayoongozwa na Nouri Al Maliki ambae ni kutoka jamii ya washia.