Ubelgiji

Hatimaye Umoja wa Ulaya EU wafikia makubaliano ya punguzo la bajeti kwa asilimia tatu

Raisi wa Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy akitangaza makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano mjini Brussels.
Raisi wa Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy akitangaza makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano mjini Brussels. REUTERS/Francois Lenoir

Viongozi wa Umoja wa Ulaya hatimaye wamefikia makubaliano juu ya bajeti ya miaka kumi baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa muda mrefu mjini Brussels,ambapo awali walitofautiana kuhusu bajeti ya Jumuiya hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy ametangaza mpango huo kwa kauli moja kuwa ni mpango unaostahili kutekelezwa.

Kwa mara ya kwanza bajeti ya umoja wa ulaya ya miaka takribani kumi imepunguzwa kwa kiasi kikubwa cha asilimia tatu.

Awali viongozi hao walitofautiana kutokana na baadhi ya nchi hususan Uingereza zikitaka mpango wa kubana matumizi ya fedha wakati Ufaransa na Italia zilipendekeza bajeti ilenge zaidi kuunda nafasi za kazi na kuinua uchumi.