MAREKANI

Rais Obama kutoa dira ya miaka minne ya Marekani

Rais wa Marekani Barrack Obama siku ya Jumanne anatarajiwa kutoa hotuba kwa taifa kuorodesha mipango yake kwa wananchi wa taifa hilo kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Matangazo ya kibiashara

Hotuba hii inakuja miezi mitatu baada ya kuchaguliwa tena kama rais wa taifa hilo na miongoni mwa maswala nyeti anayotarajiwa kuyapa kipaumbele ni pamoja na uchumi, mabadiliko ya sheria za uhamiaji, umiliki wa silaha nchini humo hasa bastola.

Wachambuzi wa siasa za Marekani wanasema kuwa hayo ndiyo mambo muhimu anayostahili kuyapa  kipaumbele kabla ya  kufanyika kwa uchaguzi  mwaka ujao.

Suala la ukosefu wa ajira pia inatarajiwa kulizungumzia na namna linavyoweza kuinua uchumi wa taifa hilo suala ambalo lililigawa taifa hilo.

 

Mbali na hotuba hiyo ya rais Obama, Wizara ya Ulinzi nchini humo imesema kuwa itawaongezea mafao wa wanandoa wa jinsia moja ambao ni wanajeshi.

Mafao hayo ni pamoja na kuwalinda watoto  hao, kuwasaidia kisheria  miongoni mwa maswala mengine ikiwemo usafiri.