VATICAN

Papa Benedicto wa XVI kuwapokea marais kufanya mazungumzo na marais watatu

REUTERS/ Max Rossi

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Benedicto wa 16 ambaye alitangaza kujiuzulu wadhifa huo kufikia mwisho wa mwezi huu anakutana na rais wa Romania Trian Basescu ,rais wa Guatemala Otto Perez, na rais wa italia Georgio Napolitano. 

Matangazo ya kibiashara

Hao ndio watakaokuwa viongozi wa mwisho kukutana na kiongozi huyo kabla ya kuacha wadhifa huo huku viongozi mbalimbali duniani wakiendelea kumpongeza katika juhudi zake za kuwaunganisha Wakristo na kuchukua uamuzi wa kuachia ngazi.

Papa Benedicto wa 16 alitangaza nia yake ya kujiuzulu mwanzoni mwa juma hili kwa sababu za kiafya na umri wake mkubwa maswala aliyoyasema yanamtatiza kuendelea na jukumu lake la kuliongoza Kanisa hilo.

Kiongozi mpya wa Kanisa hilo anatarajiwa kuchaguliwa na Makadinali kutoka nchi zote duniani mwezi ujao wa Machi kuchukua nafasi  hiyo ya ya Benedicto wa 16 raia wa Ujerumani.

Papa Benedicto mwenye umri wa miaka 85 anakuwa kiongozi wa kwanza katika miaka ya hivi karibuni kujiuzulu jambo ambalo liliwashangaza waumini wa Kanisa hilo duniani, na mapema hili akatoa wito kwa Wakristo duniani kumwombea.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa wakati umefika kwa kiongozi mpya wa kanisa hilo kutoka nje ya bara la Afrika huku Kadinali Peter Appiah Turkson wa Ghana akipewa nafasi kubwa ya kumrithi Papa Benedicto wa 16.