OSLO

Raia wa Rwanda ahukumiwa jela miaka 21 na Mahakama ya Norway.

Mahakama moja nchini Norway imemhukumu  raia mmoja wa Rwanda kifungo cha miaka 21 jela kufuatia kuhusika kwake na  mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya jijini Oslo imemkuta na hatia Sadi Bugingo ambaye amekuwa akiishi  nchini Norway kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi .

Bugingo mwenye umri wa miaka 47 amekutwa na makos ya kuchangia katika mauaji ya mamia ya watutsi katika matukio matatu tofauti, ambapo majaji wa mahakama ya jijini Oslo.

Imebainika kuwa wakati wa mauaji hayo, mtuhumiwa hakufanya lolote kuzuia mauaji hayo, na alikuwa na jukumu la kuhakikisha mauaji hayo yanatekelezwa kama ilivyopangwa.

Mauaji hayo yalitokea nchini Rwanda mwaka 1994 wakati kundi la Wanyarwanda wa kabila la Watutsi walipokimbilia katika kanisa moja la kikatoli na wengine katika hospitali moja nchini Rwanda.

Wakili wa mtuhumiwa huyo ametupilia mbali tuhuma hizo akiitaka mahakama kumuachia hutu mteja wake.