ITALIA-MAREKANI

Barack Obama na Rais wa Italia Giorgio Napolitano wazungumzia uchaguzi mkuu ujao nchini Italia

Raisi wa Marekani Barack Obama amefanya mazungumzo na Raisi wa Italia Giorgio Napolitano wakati huu ambapo Italio ipo katika maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Présidence - italienne
Matangazo ya kibiashara

Raisi Obama amesema kuwa hamu yake kubwa ni kusikia jinsi mshirika wake atakavyosimamia uchaguzi vizuri na uundwaji wa serikali kwa kuwa Italia imekuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa bara zima la Ulaya.

Aidha Rais Napolitano ameeleza kuwa nchi yake ambayo imekuwa mhanga wa madeni ni lazima iendelee na mipango endelevu kwa kuwa bado ina mahitaji muhimu kama ambavyo Ulaya na dunia pia inahitaji.

Kura za maoni zimeendelea kuonyesha kuwa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Silvio Berlusconi ambaye ameingia katika kinyang'anyiro cha Uwaziri Mkuu kwa mara nyingine amepunguza pengo kati ya chama chake cha mrengo wa kushoto kabla ya uchaguzi wa Februari 24-25.

Napolitano, ambaye anafikia ukingoni mwa uongozi wake alisema kuwa hatua za muhimu zilizochukuliwa na nchi hiyo kwa kipindi cha miezi 14 iliyopita ni lazima ziendelezwe baada ya uchaguzi wa february 24 na 25.