LIBYA

Jeshi nchini Libya laimarisha ulinzi katika siku za maadhimisho ya miaka miwili ya mapinduzi

Kiongozi wa zamani wa Libya Moammer Gaddafi,ambaye aliondolewa madarakani kwa mapinduzi yaliyofanywa na raia nchini humo.
Kiongozi wa zamani wa Libya Moammer Gaddafi,ambaye aliondolewa madarakani kwa mapinduzi yaliyofanywa na raia nchini humo. rfi

Majeshi ya Ulinzi nchini Libya yameimarisha ulinzi zaidi katika siku ambazo taifa hilo la Afrika kaskazini linaadhimisha miaka miwili tangu kuanza kwa harakati zilizomwondoa madarakani kiongozi wa zamani kanali Moammer Gaddafi.

Matangazo ya kibiashara

Raia hao walipeperusha bendera huku kauli mbiu mbalimbali zikisikika kuyasifu mapinduzi ya libya wakati magari yalizunguka mijini humo kama sehemu ya shangwe hizo sambamba na ving'ora kusikika.

Huko Benghazi raia walimiminika barabarani wakifanya matembezi ya pamoja wakikumbukia siku na eneo ambalo harakati hizo zilianzia mnamo miaka miwili iliyopita wakiwasifu walioaga dunia na kujeruhiwa katika harakati za kuumaliza utawala wa kanali Gaddafi.

Maadhimisho ya mapigano ambayo yalimalizika kwa mauaji ya Kadhafi mnamo Oktoba 2011 yanakuja wakati utawala mpya wa Libya ukikabiliwa na vita mpya dhidi ya wakosoaji ambao wametoa wito wa kufanyika mapinduzi mapya na kuushutumu utawala kushindwa kutekeleza suala la mageuzi walilolihitaji.