Pakistani

shambulizi la bomu laua 63 Pakistan

Takribani watu 63 wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya 180 wamejeruhiwa katika shambulizi la bomu eneo la Queta kusini magharibi mwa Pakistan.

Mashambulizi kadhaa ambayo yametekelezwa katika eneo la Hazara yamesababisha mamia ya watu kupoteza maisha
Mashambulizi kadhaa ambayo yametekelezwa katika eneo la Hazara yamesababisha mamia ya watu kupoteza maisha REUTERS/Naseer Ahmed
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo linatajwa kuwa la pili kwa ukubwa kutokea katika soko lenye msongamano wa watu wa jamii ya Hazara katika kipindi cha wiki tano.

Aidha mashambulizi mengine mawili yalitekelezwa katika kilabu mnamo mwezi wa kwanza tarehe 10 na kuua watu 92 huku 121 wakijeruhiwa.

Kikundi cha wapiganaji wa kiSuni Lashkar-e-Jhangvi ambacho kimepigwa marufuku nchini humo kilidai kuhusika na shambulizi la january kimeripotiwa pia kuhusika na shambulizi hilo.